Dada Jesca

Dada Jesca.

Haya sasa wadau. Hatimaye kitabu cha kwanza cha hadithi tamu ya mapenzi ya Dada Jesca-1 kimetoka. Kinaingia rasmi sokoni Jumatatu hii ya tarehe 4 April 2016, jipatie nakala yako.

Size;   Kurasa 50 za A6.

Bei;     Tsh. 3,000/=

Weka Order yako sasa na utaletewa kitabu kokote uliko.

Wasiliana nami kwa 0655 242960 na 0757 242960.

ANGALIZO: Hakifai kwa wenye umri chini ya miaka 18. Weka mbali na watoto.

SIMULIZI KUTOKA JIKONI-2

DADA JESCA APAKATWA NA SHEMEJIYE JIKONI – WAFUMANIWA.

Mtunzi; Issa S. Kanguni 0655242960

Simu iliita Da’Jesca akiwa bado kitandani hajaamka. Ni siku ya jumapili, siku ya mapunziko kwa waatumisi wa nafasi kama yake. Yeye ni katibu muhtasi, pia ni mhazini kwenye shirika moja la kiserikali lenye ofisi zake kwenye jengo la JM Mall lililopo Samora Avenue kakikati ya jiji la Dar es Salaam. Alipepesa macho kisha akageuza kichwa upande kuangalia saa ya ukutani. Inakaribia saa mbili unusu. Mwili aliuhisi mchovu kwani jana alikunywa bia zaidi ya nne wakati kiwango chake cha kawada ni chini ya bia tatu na akalala saa nane wakati kiwango chake cha kawaida ni si zaidi ya saa sita. Alikuwa akimsubiri mumewe ambaye alitarajiwa kurejea toka safari jioni ya jana. Aliangalia tamthiliya TBC na baadaye Bongo Movie.

Baada ya muito wa tatu alinyoosha mkono na kuichukua simu kwenye stuli kando ya kitanda. Alihisi ni mume wake, lakini alipoangalia jina la mpigaji, alitabasamu. Alijikohoza kusafisha koo. Akapokea. Continue reading

Simulizi Kutoka Jikoni – 1

DADA JESCA AUNGA MBOGA AKIWA MTUPU… YAWA TAMU KUPITA KAWAIDA

Mtunzi: Issa S. Kanguni, Dar es Salaam 2014

Ni ijumaa ya mwisho ya mwezi huu wa tano,  watumishi wa umma na sisi wa sekta binafsi sote  tumejidamka zetu makazini kama kawa, si unajua tena… mambo ya  kuwajibika. Mambo yote yamekwenda sawa, ila tu kwa kutimiza wajibu wangu mwingine usio rasmi, nachelea kuwadokolea kidogo yaliyojiri. Ni stori inayomhusu Dada Jesca, mhazini wetu pale ofisini.

Kisa kilianza kwa kuwa aliwahi kutoka kazini kuliko ilivyo kawaida yake, na kama ilivyo ada ya kamera yetu ya simulizi kutoka jikoni ikamfuatilia kujua kulikoni ?!! Si unajua tena…

Basi siku ile, kwanza Dada Jesca alikuja akiwa ameupara na kupendeza kwelikweli ingawa kwa kweli maumbile ya mtoto wa kike huyu hata akivaa maturubai anavutia, pili aliomba ruhusa mapema sana aweze kurudi nyumbani kwa kuvunga kuwa eti anajisika vibaya, mmh… kumbe mumewe alikuwa yu njiani kurudi toka safari ya wiki tatu na alikuwa ana hamu naye kupita maelezo. Tukumbuke kuwa ni miezi miwili tu imepita tangu Dada Jesca alipofunga pingu za maisha na kijana Badi na kuanza naye maisha mapya, kwenye nyumba mpya. Mume wake ni mfanyibiashara na alikuwa safarini kwa kipindi cha wiki tatu zilizopita.

Continue reading